Aug 16, 2017

I have learnt that caring too much on how your message will be conveyed unaweza kujikuta unabaki bubu. I’m a victim, you too at some point in your life kuna watu hawakukuelewa.

Inawezekana ilikucost kutokana na watu kutoelewa meseji yako but why care soo much???? Unless it’s a paper work, thesis or job application letter… never worry because each of us choose to interpret what suits the situations we are inn.

Sep 3, 2016

Mji wa kale uliozama kuwa kivutio Mafia
Kisiwa cha Mafia kipo katika mlango wa Mto Rufiji kusini mwa Tanzania. Maeneo ya kuvutia ya mazingira ya bahari yametokea kujulikana zaidi haswa mara baada ya kuanzishwa Hifadhi ya Bahari (Mafia Island Marine Park - MIMP) na Maeneo Tengefu.
Kisiwa hiki kipo umbali wa kilomita 135 kutoka Dar es Salaam na huchukua dakika 35 kwa kutumia ndege ndogo kufika hapo.
Unapotafuta habari za Kisiwa cha Mafia kwenye mitandao hukupeleka kwenye taarifa za vivutio vya utalii pekee ambavyo vinajenga sura ya kisiwa hiki kuwa ni pepo ya watalii. 
Kisiwa hiki ni sehemu ya wilaya sita za mkoa wa Pwani. Kinachokadiriwa kuwa na wakazi 40,800 wanaotegemea kilimo na uvuvi.
Kutokana na historia kinavutia watalii wanaofika kisiwani humo kwaajili ya fungate, kutazama pomboo na uvuvi wa kujirufahisha.
Hivi karibuni karibuni katika kisiwa hiki ambacho historia yake iliyo katika maandishi inaanzia karne ya nane, kilipamba vichwa vya habari baada ya kugundulika uwepo wa mji uliozama baharini.
Habari hii iliibua mjadala huku upande mmoja ukisema inawezekana kweli mji huo ulizama na mwingine ukisema ni maajabu tu ya Mungu na kwamba maji yametengeneza mfano wa mji.
Mjadala huu unazidi kukitangaza Kisiwa hiki na utazidi kuvutia watalii kutoka kila kona ya dunia kujionea ajabu hili.
Ugunduzi huo unaonekana utakuza zaidi utalii kwa kuwa watafiti wanamiminika na watalii vilevile kila mmoja akitaka kupata ukweli.
Wengine wanasema inawezekana mji huo ulizama miaka 500 kutokana na mwonekano wa matumbawe yaliyojipachika katika kuta zilizoanguka.
Lakini mtandao wa Ancient-origins unasema inawezekana mji huo ni Raphta uliokuwa ukikaliwa na Warumi katika karne  ya kwanza
Mtandao huo unamnukuu Mtaalamu wa Mambo ya Kale ambaye ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Felix Chami kuwa muonekano wa mabaki hayo unafanana na maelezo yaliyopo katika nyaraka za Warumi.

Mji wa Raphta ambao ulikuwa maarufu kwa biashara katika karne ya kwanza, ulionekana katika nyaraka na kwa miaka mingi wataalamu wa kale wamekuwa wakitafuta ukweli.
Kwa mujibu wa Allan Sutton baada ya kuruka na helikopta aliona uwapo kitu kisicho cha kawaida na kwamba maji yalikuwa yakigawanyika kwa namna iliyompa shauku ya kutaka kujua zaidi.

Sutton na wenzake baadaye walifanikiwa kulitembelea eneo hilo  wakati wa maji kupwa wakiwa na mashua na vifaa vya kupiga mbizi na kufanikiwa kulichunguza na kulipiga picha.
Katika utafiti wao huo waliona kitu kinachoonekana kama misingi inayozunguka eneo kubwa. Katika misingi hiyo kulionekana kuta kubwa za sarufi za mita tano na zaidi.
Msingi wa majengo hayo upande wa kaskazini na kusini una wastani wa kati ya urefu wa kilometa 3.7  ila wanaamini kwamba kuna misingi mingine ambayo hawakuiona ambayo imefunikwa na mchanga. Na hatua zaidi za kitaalamu zinatakiwa kuchukuliwa ili kubaini hali ya hapo.
Anasema katika blogu yake kwamba katika maeneo mengine upo upana mkubwa wa kiasi cha kilometa moja huku kina chake kikiwa ni kati ya mita 12 hadi 20.
 Sutton anasema kuta zinafanana na mchanga lakini ukitazama karibu ni kama vile zimejengwa na saruji na katika kumeonekana matundu ambayo huenda ni madirisha au milango.


iPhone 7 to hit the market 

Wapenzi wa simu za mkononi hasa zinazotengenezwa na Kampuni ya Apple wanafahamu kuwa Septemba 6 mwaka huu historia nyingine itatengenezwa.
Siku hii inatarajiwa kuwa kampuni hiyo itazindua simu mpya aina ya iPhone 7, iPhone Plus na saa za Apple Watch 2.
Tetesi zilikuwepo kuwa kampuni hiyo inaandaa shughuli kubwa itakayofanyika Jumatano ya kwanza ya Septemba  katika Jiji la San Fransisco.
Ingawa simu hizo zinatarajiwa kuzinduliwa Septemba 7, inaelezwa kuwa zitakuwa madukani katika nchi zote kuanzia Septemba 16 mpaka 23.
Tetesi zinaeleza kuwa simu hiyo itakuwa kama ifuatavyo
·         Upana wa inchi 4.7 na urefu wa inchi 5.5 na hii ni kwa simu zote yaani iPhone 7 na iPhone 7 Plus.
·         Mwonekano wake hautakuwa tofauti na simu za iPhone 6 lakini inaelezwa kuwa haitakuwa na button ya kuanzia (home button)
·         Simu hizi zitakuwa na kamera kubwa iliyoongezwa uwezo wa kutoa picha nzuri.
·         Tetesi nyingine zinasema simu hizi hazitakuwa na tundu la kuwekea headphones na kwamba itatumia zile zisizo na waya.
·         Button ya kuanzia itakuwa ya kupapasa (touch screen)
·         Itakuwa na uwezo wa kuhifadhi kumbukumbu kati ya GB32 na GB256
·         Itakuwa na kasi ya A10 processor.
·         Itaendeshwa kwa mfumo iOS 10 
·         Itakuwa na uwezo wa kuzuia maji kuingia (water resistance)
·         Spika za kusikilizia muziki na sauti zimeboreshwa zaidi


Jul 9, 2016

We all got 24 hrs, be the best you can be


Unaweza kudhani mwenzako anapewa saa 24 halafu wewe una 12 kwa sababu muda huwa haukutoshi. Kila kitu chako hakikamiliki kwa wakati.
Hebu kumbuka wakati unasoma, unaweza kujikuta unafua sare zako Jumapili jioni. Jumatatu unalazimika kwenda shule hujachana nywele na hujanyoosha nguo kwa sababu muda haukuruhusu.
Unaingia darasani unatweta kwa kuwa ulikimbia kuwahi lakini pia unagundua haraka hizo zimekufanya usahau kubeba baadhi ya madaftari na wakati mwingine kalamu.
Mpaka unamaliza elimu yako ya sekondari hukumbuki siku ambayo ulikwenda shule ukitembea au kipindi cha mitihani kikukute umeshajisomea. Siku zote ulianza kusoma baada ya kuiona ratiba ya mitihani kwenye mbao za matangazo.
Bahati mbaya tabia hii umekuwa nayo  mpaka sasa. Hujawahi kufika kwenye mkutano, kazini, kwenye ibada kwa wakati na inapotokea hivyo huwa umekimbizana kuwahi.
Unakuwa bingwa wa kuomba udhuru kwa sababu ambazo mwingine hawezi kuzifikiria. Ukishakomaa katika chelewachelewa huishiwi na misemo ya foleni ndefu, mara gari liliharibika au ghafla unapigiwa simu ya mgonjwa.
Ukipiga hesabu ya visingizio vyako utadungua kuwa kwa mwezi unapanda magari mabovu mara mbili, unauguliwa na ndugu hewa,  viatu vinakatika, unashikwa na tumbo la ghafla na kila aina ya kisingizio kinachokujia kichwani.
Ndiyo maana hata kwenye sherehe na matamasha tunayohudhuria huwa ratiba zake zinakwenda kinyume. Chakula kitachelewa kufika ukumbini na kikiwahi utasikia sahani zimesahaulika Mbezi na sherehe inafanyika Upanga.
Ahadi za matasha kumalizika saa sita usiku sasa imeshazoeleka kuwa ni za uongo, kwa sababu wasanii huingia ukumbini saa saba tena baada ya kutafutwa kwa tochi.
Kuwa ‘mtu wa dakika za mwisho’ kumesababisha wasanii wengi kushuka kimuziki. Wapo wale ambao walikuwa wakilalamikiwa waziwazi na waandaaji matamasha na mashabiki lakini mwishowe waliamua kuchana nao.
Watu wengi wanatabia hii isipokua zinapishana kiwango. Kama unavyojaribu kutibu maradhi mengine hili nalo linapaswa kuondolewa.
La muhimu kuliko yote ni kujifunza thamani ya muda. Yaani jiulize ule muda ambao hujiandaa kwa ratiba iliyo mbele yako unautumiaje?
Unaweza kuchelewa jambo kwa kuwa ulikuwa umetingwa na kitu kingine, inapotokea ukachelewa tu huku huwa na jambo la msingi unalofanya hesabu kuwa upo katika matatizo.
Hata mimi nina ugonjwa huu lakini ninautibia hivi sasa,  hivyo nimeona siyo vibaya kuwakumbusha wenzangu.

Jun 25, 2016

                                                                 Mark Wahlberg 



                                     Mark Wahlberg alikuwa muuza ‘unga’
Mcheza sinema huyu ni mfano hai kuwa unapoanguka katika uovu unaweza kuinuka na kufanya maajabu.
Mwigizjai wa Mark Wahlberg aliwahi kuhukumiwa kifungo cha miaka 10 jela baada ya kupatikana na hatia ya kufanya biashara ya dawa za kulevya na kutishia kuua.
Bahati ilikuwa yake kwani alitumikia siku 45 tu katika gereza lenye ulinzi mkali huko Marekani.

“Siku 45 nilizokaa gerezani zilinifungua kuwa ninaweza kuwa mwigizaji  wa filamu, nilipotoka niliamua kubadilika,” anasema.

BREXIT BREXIT BREXIT







Unataka Tanzania ikukumbuke kwa lipi zuri ulilolifanya?

Tanzanian'n flag
Kwanza niseme mapema, huwa sipendi kuandika kuhusu kufa ndio maana nimechagua  mada hii leo. Tuache habari za kukumbukwa baada ya kifo, bali uenziwe ukiwa hai.
Lady Jay Dee waliwahi kuimba kuwa kuna watu wana historia hata kabla hawajaiaga dunia lakini ni zile mbaya zisizofaa kuigwa.
Nimesema sipendi kuzungumzia kifo ingawa hakikwepeki kwa kuwa kinakamilisha ubinadamu wetu, acha tu nikiongelee katika aya moja inayofuata.
Anyooshe mkono mtu ambaye amewahi kusikia wasifu mbaya wa marehemu katika msiba…Hakika mazingira yanatulazimisha kukumbuka yale mawili matatu mema aliyotenda na haya husaidia kutoa faraja.
Ni vigumu kuwa mkamilifu. Kuna watu utawakwaza tu kwa sababu ya namna unavyotembea au kutafuna chakula. Wapo watakaokwazika na namna unavyozitumia kurasa zako katika mitandao ya kijamii.
Utamsikia mtu anasema: “Simpendi jamaa anaandika pumba yule”. Hizi ni tofauti za kibinadamu, unachoona sahihi mwenzako anaona kichefuchefu.
Lakini yapo mambo makuu ya msingi ambayo kutokana na rika unapaswa kuyafanya kwa ajili yako, familia yako na taifa kwa ujumla.
Unapokuwa mdogo wajibu wako ni kusoma na kuwa na heshima kwa jamii nzima. Kuna usemi wa mtaani kuwa unapokuwa mdogo unaishi kwa kutegemea shikamoo. Yaani wewe unalipa kodi zote kwa kusalimia tu.
Huo ni wajibu na hubadilika kutokana na umri. Unapomaliza elimu ya juu unatakiwa kulitumia taifa kwa kufanya kazi kwa bidii na kuzalisha.
Unawajibika kulipa kodi na kufanya shughuli nyingine za kijamii kama kusaidia wasiojiweza na wazee. Huu ndio wakati wa kufanya mambo mengine mengi ya kihistoria.
Unaweza kufanya uvumbuzi wa kitu au jambo na kwenye vipaji huu ndio wakati wa kuvitumikia ingawa vinatakiwa kuwa vilianza kulelewa tangu utotoni. Mark Zuckerberg aligundua Facebook akiwa katika rika hili.
Kwa mazingira yetu hali ni tofauti kipaji unakuwa nacho kitachanua mbele ya safari ka juhudi zako binafsi.
Wakati huu ni mbaya pia na wengi wanaishia hapa. Unapokuwa na pesa ni rahisi kuingia kwenye vishawishi vingine na kitabu kinaweza kubadilika kuwa na kurasa zisizovutia kusoma.
Vijana kama Hellen Dausen, Millard Ayo, Flaviana Matata, wapo katika hatua hii.  Wanahistoria zao tayari. Tukiziandika leo hii hakika ni za kufurahisha na pengine walimu wanaweza kuzitumia kufundisha masomo ya elimu ya uraia.
Wajibu hujenga historia kama ikifuatwa vile inavyotakiwa. Kila mmoja anaweza kujiwekea historia akiwa hai. 


I have learnt that caring  too much on how your message will be conveyed unaweza kujikuta unabaki bubu. I’m a victim, you too at some poi...