Jun 25, 2016

Unataka Tanzania ikukumbuke kwa lipi zuri ulilolifanya?

Tanzanian'n flag
Kwanza niseme mapema, huwa sipendi kuandika kuhusu kufa ndio maana nimechagua  mada hii leo. Tuache habari za kukumbukwa baada ya kifo, bali uenziwe ukiwa hai.
Lady Jay Dee waliwahi kuimba kuwa kuna watu wana historia hata kabla hawajaiaga dunia lakini ni zile mbaya zisizofaa kuigwa.
Nimesema sipendi kuzungumzia kifo ingawa hakikwepeki kwa kuwa kinakamilisha ubinadamu wetu, acha tu nikiongelee katika aya moja inayofuata.
Anyooshe mkono mtu ambaye amewahi kusikia wasifu mbaya wa marehemu katika msiba…Hakika mazingira yanatulazimisha kukumbuka yale mawili matatu mema aliyotenda na haya husaidia kutoa faraja.
Ni vigumu kuwa mkamilifu. Kuna watu utawakwaza tu kwa sababu ya namna unavyotembea au kutafuna chakula. Wapo watakaokwazika na namna unavyozitumia kurasa zako katika mitandao ya kijamii.
Utamsikia mtu anasema: “Simpendi jamaa anaandika pumba yule”. Hizi ni tofauti za kibinadamu, unachoona sahihi mwenzako anaona kichefuchefu.
Lakini yapo mambo makuu ya msingi ambayo kutokana na rika unapaswa kuyafanya kwa ajili yako, familia yako na taifa kwa ujumla.
Unapokuwa mdogo wajibu wako ni kusoma na kuwa na heshima kwa jamii nzima. Kuna usemi wa mtaani kuwa unapokuwa mdogo unaishi kwa kutegemea shikamoo. Yaani wewe unalipa kodi zote kwa kusalimia tu.
Huo ni wajibu na hubadilika kutokana na umri. Unapomaliza elimu ya juu unatakiwa kulitumia taifa kwa kufanya kazi kwa bidii na kuzalisha.
Unawajibika kulipa kodi na kufanya shughuli nyingine za kijamii kama kusaidia wasiojiweza na wazee. Huu ndio wakati wa kufanya mambo mengine mengi ya kihistoria.
Unaweza kufanya uvumbuzi wa kitu au jambo na kwenye vipaji huu ndio wakati wa kuvitumikia ingawa vinatakiwa kuwa vilianza kulelewa tangu utotoni. Mark Zuckerberg aligundua Facebook akiwa katika rika hili.
Kwa mazingira yetu hali ni tofauti kipaji unakuwa nacho kitachanua mbele ya safari ka juhudi zako binafsi.
Wakati huu ni mbaya pia na wengi wanaishia hapa. Unapokuwa na pesa ni rahisi kuingia kwenye vishawishi vingine na kitabu kinaweza kubadilika kuwa na kurasa zisizovutia kusoma.
Vijana kama Hellen Dausen, Millard Ayo, Flaviana Matata, wapo katika hatua hii.  Wanahistoria zao tayari. Tukiziandika leo hii hakika ni za kufurahisha na pengine walimu wanaweza kuzitumia kufundisha masomo ya elimu ya uraia.
Wajibu hujenga historia kama ikifuatwa vile inavyotakiwa. Kila mmoja anaweza kujiwekea historia akiwa hai. 


No comments:

I have learnt that caring  too much on how your message will be conveyed unaweza kujikuta unabaki bubu. I’m a victim, you too at some poi...