Sep 3, 2016

Mji wa kale uliozama kuwa kivutio Mafia
Kisiwa cha Mafia kipo katika mlango wa Mto Rufiji kusini mwa Tanzania. Maeneo ya kuvutia ya mazingira ya bahari yametokea kujulikana zaidi haswa mara baada ya kuanzishwa Hifadhi ya Bahari (Mafia Island Marine Park - MIMP) na Maeneo Tengefu.
Kisiwa hiki kipo umbali wa kilomita 135 kutoka Dar es Salaam na huchukua dakika 35 kwa kutumia ndege ndogo kufika hapo.
Unapotafuta habari za Kisiwa cha Mafia kwenye mitandao hukupeleka kwenye taarifa za vivutio vya utalii pekee ambavyo vinajenga sura ya kisiwa hiki kuwa ni pepo ya watalii. 
Kisiwa hiki ni sehemu ya wilaya sita za mkoa wa Pwani. Kinachokadiriwa kuwa na wakazi 40,800 wanaotegemea kilimo na uvuvi.
Kutokana na historia kinavutia watalii wanaofika kisiwani humo kwaajili ya fungate, kutazama pomboo na uvuvi wa kujirufahisha.
Hivi karibuni karibuni katika kisiwa hiki ambacho historia yake iliyo katika maandishi inaanzia karne ya nane, kilipamba vichwa vya habari baada ya kugundulika uwepo wa mji uliozama baharini.
Habari hii iliibua mjadala huku upande mmoja ukisema inawezekana kweli mji huo ulizama na mwingine ukisema ni maajabu tu ya Mungu na kwamba maji yametengeneza mfano wa mji.
Mjadala huu unazidi kukitangaza Kisiwa hiki na utazidi kuvutia watalii kutoka kila kona ya dunia kujionea ajabu hili.
Ugunduzi huo unaonekana utakuza zaidi utalii kwa kuwa watafiti wanamiminika na watalii vilevile kila mmoja akitaka kupata ukweli.
Wengine wanasema inawezekana mji huo ulizama miaka 500 kutokana na mwonekano wa matumbawe yaliyojipachika katika kuta zilizoanguka.
Lakini mtandao wa Ancient-origins unasema inawezekana mji huo ni Raphta uliokuwa ukikaliwa na Warumi katika karne  ya kwanza
Mtandao huo unamnukuu Mtaalamu wa Mambo ya Kale ambaye ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Felix Chami kuwa muonekano wa mabaki hayo unafanana na maelezo yaliyopo katika nyaraka za Warumi.

Mji wa Raphta ambao ulikuwa maarufu kwa biashara katika karne ya kwanza, ulionekana katika nyaraka na kwa miaka mingi wataalamu wa kale wamekuwa wakitafuta ukweli.
Kwa mujibu wa Allan Sutton baada ya kuruka na helikopta aliona uwapo kitu kisicho cha kawaida na kwamba maji yalikuwa yakigawanyika kwa namna iliyompa shauku ya kutaka kujua zaidi.

Sutton na wenzake baadaye walifanikiwa kulitembelea eneo hilo  wakati wa maji kupwa wakiwa na mashua na vifaa vya kupiga mbizi na kufanikiwa kulichunguza na kulipiga picha.
Katika utafiti wao huo waliona kitu kinachoonekana kama misingi inayozunguka eneo kubwa. Katika misingi hiyo kulionekana kuta kubwa za sarufi za mita tano na zaidi.
Msingi wa majengo hayo upande wa kaskazini na kusini una wastani wa kati ya urefu wa kilometa 3.7  ila wanaamini kwamba kuna misingi mingine ambayo hawakuiona ambayo imefunikwa na mchanga. Na hatua zaidi za kitaalamu zinatakiwa kuchukuliwa ili kubaini hali ya hapo.
Anasema katika blogu yake kwamba katika maeneo mengine upo upana mkubwa wa kiasi cha kilometa moja huku kina chake kikiwa ni kati ya mita 12 hadi 20.
 Sutton anasema kuta zinafanana na mchanga lakini ukitazama karibu ni kama vile zimejengwa na saruji na katika kumeonekana matundu ambayo huenda ni madirisha au milango.


No comments:

I have learnt that caring  too much on how your message will be conveyed unaweza kujikuta unabaki bubu. I’m a victim, you too at some poi...