iPhone 7 to hit the market
Wapenzi
wa simu za mkononi hasa zinazotengenezwa na Kampuni ya Apple wanafahamu kuwa
Septemba 6 mwaka huu historia nyingine itatengenezwa.
Siku
hii inatarajiwa kuwa kampuni hiyo itazindua simu mpya aina ya iPhone 7, iPhone
Plus na saa za Apple Watch 2.
Tetesi
zilikuwepo kuwa kampuni hiyo inaandaa shughuli kubwa itakayofanyika Jumatano ya
kwanza ya Septemba katika Jiji la San
Fransisco.
Ingawa
simu hizo zinatarajiwa kuzinduliwa Septemba 7, inaelezwa kuwa zitakuwa madukani
katika nchi zote kuanzia Septemba 16 mpaka 23.
Tetesi
zinaeleza kuwa simu hiyo itakuwa kama ifuatavyo
·
Upana
wa inchi 4.7 na urefu wa inchi 5.5 na hii ni kwa simu zote yaani iPhone 7 na
iPhone 7 Plus.
·
Mwonekano
wake hautakuwa tofauti na simu za iPhone 6 lakini inaelezwa kuwa haitakuwa na
button ya kuanzia (home button)
·
Simu
hizi zitakuwa na kamera kubwa iliyoongezwa uwezo wa kutoa picha nzuri.
·
Tetesi
nyingine zinasema simu hizi hazitakuwa na tundu la kuwekea headphones na kwamba
itatumia zile zisizo na waya.
·
Button
ya kuanzia itakuwa ya kupapasa (touch screen)
·
Itakuwa
na uwezo wa kuhifadhi kumbukumbu kati ya GB32 na GB256
·
Itakuwa
na kasi ya A10 processor.
·
Itaendeshwa
kwa mfumo iOS 10
·
Itakuwa
na uwezo wa kuzuia maji kuingia (water resistance)
·
Spika
za kusikilizia muziki na sauti zimeboreshwa zaidi
No comments:
Post a Comment