Avic Town:
My Dar es Salaam, My New Tanzania
The entrance |
Kama
ingetokea watu wakakubeba ukiwa usingizini na kukuacha katika eneo hili, hakika
utakapoamka utasema “nataka niendelee kuishi hapa”, au labda ungeweza kusema:
“Sirudi tena Tanzania, nitaendelea kuishi nchi hii,”.
Lakini hapa
siyo Johannesburg, Afrika Kusini wala siyo Algiers, Algeria. Hapa ni Kigamboni
jijini Dar es Salaam. Ni mwendo wa Kilomita 25 tu kutoka katikati ya Jiji la
Dar es Salaam.
Inawezekana
umeshawahi kuwa na ndoto ya kuishi mahali utakapojivunia kupaita nyumbani, eneo
unalotamani kuona watoto wako wakikua kwa amani, sehemu itakayokuondolea msongo
wa mawazo. Hapa ndiyo sehemu ya kupata mwafaka wa matamanio yako.
Moja ya
mabango katika eneo hilo limeandikwa A
place that gives you a peace of mind likimaanisha eneo ambalo linakupa
tulizo la moyo wako. Kama unaishi hapa hakika utatulia lakini kama ni mpita
njia utapata wakati mgumu kuaga.
Unapoingia
katika eneo hili unakutana na barabara safi ya lami. Kutokana na mji
ulivyojengwa. Kulia kwa geti hili kuna viwanja viwili vya michezo. Kipo kiwanja
cha mpira wa miguu na kikapu.
Mbele
zinaonekana nyumba zilizopangwa kwa ustadi wa hali ya juu. Siyo aina ya nyumba
ambazo zipo katika miji yetu-mijini au vijijini.
Kutokana na
hali halisi hasa za kiusalama, nyumba nyingi mijini zimezungushiwa kuta kubwa
kila moja ikiwa na rangi yake hali ambayo hifanya mitaa kuonekana michafu.
Nyumba hizi
zimetenganishwa kwa fensi ya nyaya inayowezesha upepo kupenya vyema. Upepo
unapenya vyema na kuitofautisha hali ya hewa na maeneo mengi ya jijini la Dar
es Salaam.
Mitaa yake
haina mchanga lakini imesheheni kijani kibichi. Majani yameoteshwa kwa ustadi
wa hali ya juu na kujengewa kwa vitofali
pembeni kwa utaalamu hali inayoyafanya mazingira yake yavutie kuyatazama
wakati wote.
Maua na miti
iliyooteshwa kwa mpangilio inalifanya eneo hili kuwa na harufu nzuri. Kila
unapogeuka kuna mandhari nzuri ya kuvutia kutazama kutokana na ardhi hiyo
kufunikwa na majani yaliyopangiliwa vizuri na kulifanya eneo ambalo
halijafunikwa kwa lami au vitofali.
Such a nice place.....drooling |
Avic Town ni nini?
Huu ni mji
ambao jamii kubwa inaunganishwa katika viunga vya eneo lililopo Kigamboni
jijini Dar es Salaam pembezoni mwa fukwe za amani.
Katika awamu
ya kwanza nyumba zaidi ya 102 zimekwisha jengwa na zinauzwa kwa Watanzania tu.
Msimamizi wa
mauzo katika kijiji hicho, Lucy Makusa anasema nyumba hizo hazitauzwa kwa mgeni
labda awe ameoa au ameolewa na Mtanzania.
“Hizi nyumba
zinauzwa kwa Watanzania kwa sababu tunauza na ardhi, mgeni hawezi kununua
nyumba hapa,” anasema Makusa.
Makazi
hayawezi kukamilika bila kuwa na maeneo ya kibiashara, eneo hili pia lina eneo
kubwa la maduka ya kisasa yatakayouza bidhaa mbalimbali.
Hakuna kwenda
tena Afrika Kusini
Kwa wasanii
hasa wa muziki wa Kizazi Kipya iliwalazimu kusafiri mpaka nje ya nchi hasa
Afrika Kusini ili kupata mandhari nzuri kwa ajili ya upigaji picha za video.
Uwepo wa
eneo hili umeanza kuwaondolea adha ya wasanii nchini kwani sasa wanarekodi
nyimbo zao hapa nchini huku zikiwa na mandhari kama ya zile zilizotengenezwa
nje.
Msanii David
Genzi (Young D), Zuwena Mohamed (Shilole), Raymond Shaban (Raymond) na Baraka
Andrew (Baraka da Prince) ni baadhi ya wasanii ambao wameshaitumia fursa hiyo
kwa kurekodi nyimbo zako katika kijiji hiki.
Kama unataka
kusafiri kwa macho kutoka hapo ulipo, tazama nyimbo Nyang’anyang’a wa Shilole,
Kwetu wa Raymond au Ujanja Ujanja wa Young D utaona mandhari ya maeneo hayo.
Makusa
anasema wamekuwa wakitoa fursa kwa wasanii kurekodi nyimbo zao bila kuwatoza gharama zozote wakiamini kuwa kwa
kufanya hivyo wanawasaidia wasanii.
“Lakini pia
tunataka kuwaonyesha Watanzania kuwa kuna sehemu ambayo wanaweza kujivunia kwa
kuwa ipo katika ardhi yao,” anasema Makusa.
Zipo nyumba za aina ngapi
Makusa
anasema nyumba zipo za ukubwa mbalimbali. Nyumba za kawaida za vyumba vinne
zipo 10, za vyumba vitatu zipo 30, za vyumba viwili ambazo ujenzi wake bado
unaendelea zitakuwa 15, nyumba za ghorofa moja ambazo zitakuwa na vyumba vinne
na vitano zitakuwa 77.
Nyumba za
vyumba vitatu zimejengwa katika eneo lenye ukubwa wa mita za mraba 500, za
vyumba vinne mita za mraba 700 na zile ghorofa zimejengwa katika eneo la ukubwa
wa mita za mraba 1,000-1,500.
Ndani ya nyumba hizi
Nyumba kubwa
ni za ghorofa moja zenye vyumba sita vya kulala. Hii imepewa jina la Premium
Villa. Mbali na vyumba vya kulala ina
sebule mbili, chumba cha kuhifadhia nguo,
chumba cha kulia chakula, majiko
mawili na mabafu sita.
Aina
nyingine pia ni ya nyumba za ghorofa moja waliyooiita Family Villa ina vyumba
vitano vya kulala, sebule mbili, chumba
maalumu cha kuhifadhia nguo, mabafu manne na jiko la kisasa.
Nyumba za vyumba
vitatu ambazo zinatoshea familia nyingi za Kitanzania zina chumba kikubwa cha
kulia cha chakula, sebule kubwa, mabafu viwili na jiko moja kubwa.
The interior is to crave for |
Totauti na maeneo mengine
Wakazi wake
kila mmoja atakuwa na kadi maalumu ya kuingilia ambayo atakuwa akiisugua katika
mashine na geti litafunguka. Pia eneo hilo litalindwa saa 24 kwa mitambo ya
kisasa.
Ni eneo
ambalo mtoto anaweza kukua bila kujua adha ya kukatika kwa umeme na maji kama
ilivyo kwa maeneo yote nchini.
Makusa
anasema mazingira safi yanayoonekana sasa ndivyo yatakavyokuwa miaka 20 baadaye
kutokana na mikakati iliyowekwa ya kuhakikisha maua, majani na miti vinatunzwa
vilivyo.
Ujenzi unaendelea
Unapofika
katika eneo hilo utaona ujenzi unaendelea, moja kati ya majengo yanayoonyesha
kuwa katika hatua za mwisho mwisho ni jengo la kusambazia maji (water tower),
bwawa la kuogelea na jengo la kufanyia mazoezi.
Ujenzi
katika eneo hilo utaendelea baada ya awamu hii ya kwanza kukamilika.
Makusa
anasema hiki kilichofanyika mpaka sasa ni sawa na robo tu ya mradi mzima.
“Uwekezaji
wa hapa ni ekari 583 lakini hapa ulipopaona
ni ekari 44 tu, unaweza kutabiri ni jinsi gani hapa patakavyokuwa miaka mitano
baadaye.” Anasema Makusa.
Kampuni inayoendeleza makazi haya
Kijiji cha
Avic kinaendelezwa na Kampuni ya Avic Coast Land Development iliyo chini ya Avic International ya nchini
China.
Kampuni ya
Avic International ni mashuhuri ulimwenguni kote kwa biashara za usafiri wa anga, uchukuzi,
uendelezaji wa makazi, usimamizi wa hoteli, uuzaji wa vifaa vya umeme na huduma
za teknolojia.
ADIOS.
No comments:
Post a Comment