Unataka
Tanzania ikukumbuke kwa lipi zuri ulilolifanya?
Tanzanian'n flag |
Lady Jay Dee
waliwahi kuimba kuwa kuna watu wana historia hata kabla hawajaiaga dunia lakini
ni zile mbaya zisizofaa kuigwa.
Nimesema
sipendi kuzungumzia kifo ingawa hakikwepeki kwa kuwa kinakamilisha ubinadamu
wetu, acha tu nikiongelee katika aya moja inayofuata.
Anyooshe
mkono mtu ambaye amewahi kusikia wasifu mbaya wa marehemu katika msiba…Hakika
mazingira yanatulazimisha kukumbuka yale mawili matatu mema aliyotenda na haya
husaidia kutoa faraja.
Ni vigumu
kuwa mkamilifu. Kuna watu utawakwaza tu kwa sababu ya namna unavyotembea au
kutafuna chakula. Wapo watakaokwazika na namna unavyozitumia kurasa zako katika
mitandao ya kijamii.
Utamsikia
mtu anasema: “Simpendi jamaa anaandika pumba yule”. Hizi ni tofauti za
kibinadamu, unachoona sahihi mwenzako anaona kichefuchefu.
Lakini yapo
mambo makuu ya msingi ambayo kutokana na rika unapaswa kuyafanya kwa ajili
yako, familia yako na taifa kwa ujumla.
Unapokuwa
mdogo wajibu wako ni kusoma na kuwa na heshima kwa jamii nzima. Kuna usemi wa
mtaani kuwa unapokuwa mdogo unaishi kwa kutegemea shikamoo. Yaani wewe unalipa
kodi zote kwa kusalimia tu.
Huo ni
wajibu na hubadilika kutokana na umri. Unapomaliza elimu ya juu unatakiwa
kulitumia taifa kwa kufanya kazi kwa bidii na kuzalisha.
Unawajibika
kulipa kodi na kufanya shughuli nyingine za kijamii kama kusaidia wasiojiweza
na wazee. Huu ndio wakati wa kufanya mambo mengine mengi ya kihistoria.
Unaweza
kufanya uvumbuzi wa kitu au jambo na kwenye vipaji huu ndio wakati wa
kuvitumikia ingawa vinatakiwa kuwa vilianza kulelewa tangu utotoni. Mark Zuckerberg aligundua Facebook akiwa katika rika hili.
Kwa
mazingira yetu hali ni tofauti kipaji unakuwa nacho kitachanua mbele ya safari
ka juhudi zako binafsi.
Wakati huu
ni mbaya pia na wengi wanaishia hapa. Unapokuwa na pesa ni rahisi kuingia
kwenye vishawishi vingine na kitabu kinaweza kubadilika kuwa na kurasa
zisizovutia kusoma.
Vijana kama
Hellen Dausen, Millard Ayo, Flaviana Matata, wapo katika hatua hii. Wanahistoria zao tayari. Tukiziandika leo hii
hakika ni za kufurahisha na pengine walimu wanaweza kuzitumia kufundisha masomo
ya elimu ya uraia.
Wajibu
hujenga historia kama ikifuatwa vile inavyotakiwa. Kila mmoja anaweza kujiwekea
historia akiwa hai.
No comments:
Post a Comment