Jul 9, 2016

We all got 24 hrs, be the best you can be


Unaweza kudhani mwenzako anapewa saa 24 halafu wewe una 12 kwa sababu muda huwa haukutoshi. Kila kitu chako hakikamiliki kwa wakati.
Hebu kumbuka wakati unasoma, unaweza kujikuta unafua sare zako Jumapili jioni. Jumatatu unalazimika kwenda shule hujachana nywele na hujanyoosha nguo kwa sababu muda haukuruhusu.
Unaingia darasani unatweta kwa kuwa ulikimbia kuwahi lakini pia unagundua haraka hizo zimekufanya usahau kubeba baadhi ya madaftari na wakati mwingine kalamu.
Mpaka unamaliza elimu yako ya sekondari hukumbuki siku ambayo ulikwenda shule ukitembea au kipindi cha mitihani kikukute umeshajisomea. Siku zote ulianza kusoma baada ya kuiona ratiba ya mitihani kwenye mbao za matangazo.
Bahati mbaya tabia hii umekuwa nayo  mpaka sasa. Hujawahi kufika kwenye mkutano, kazini, kwenye ibada kwa wakati na inapotokea hivyo huwa umekimbizana kuwahi.
Unakuwa bingwa wa kuomba udhuru kwa sababu ambazo mwingine hawezi kuzifikiria. Ukishakomaa katika chelewachelewa huishiwi na misemo ya foleni ndefu, mara gari liliharibika au ghafla unapigiwa simu ya mgonjwa.
Ukipiga hesabu ya visingizio vyako utadungua kuwa kwa mwezi unapanda magari mabovu mara mbili, unauguliwa na ndugu hewa,  viatu vinakatika, unashikwa na tumbo la ghafla na kila aina ya kisingizio kinachokujia kichwani.
Ndiyo maana hata kwenye sherehe na matamasha tunayohudhuria huwa ratiba zake zinakwenda kinyume. Chakula kitachelewa kufika ukumbini na kikiwahi utasikia sahani zimesahaulika Mbezi na sherehe inafanyika Upanga.
Ahadi za matasha kumalizika saa sita usiku sasa imeshazoeleka kuwa ni za uongo, kwa sababu wasanii huingia ukumbini saa saba tena baada ya kutafutwa kwa tochi.
Kuwa ‘mtu wa dakika za mwisho’ kumesababisha wasanii wengi kushuka kimuziki. Wapo wale ambao walikuwa wakilalamikiwa waziwazi na waandaaji matamasha na mashabiki lakini mwishowe waliamua kuchana nao.
Watu wengi wanatabia hii isipokua zinapishana kiwango. Kama unavyojaribu kutibu maradhi mengine hili nalo linapaswa kuondolewa.
La muhimu kuliko yote ni kujifunza thamani ya muda. Yaani jiulize ule muda ambao hujiandaa kwa ratiba iliyo mbele yako unautumiaje?
Unaweza kuchelewa jambo kwa kuwa ulikuwa umetingwa na kitu kingine, inapotokea ukachelewa tu huku huwa na jambo la msingi unalofanya hesabu kuwa upo katika matatizo.
Hata mimi nina ugonjwa huu lakini ninautibia hivi sasa,  hivyo nimeona siyo vibaya kuwakumbusha wenzangu.

No comments:

I have learnt that caring  too much on how your message will be conveyed unaweza kujikuta unabaki bubu. I’m a victim, you too at some poi...